'WHERE IS MY MISS AJAKAYE?' BY ARTYST MSAFIH POETICS.
Ukutani picha
Chumbani picha
Akilini picha
Hadi kwenye simu Ni yako picha
Ama kweli nashindwa kuficha
Urembo wako unaniwacha kicha'
Nakumbuka pale tulipokutana
Mjini dar-esalam... Uzuri wako ulininata
Mawazo ukani kamata
Swadakta...
Angalau sauti tamu
Kanipa hamu ya kukufahamu...
Kwa kina
Nikitizama zako picha
Nabaki kicha'
Hadi sipati lepe...usingizi kuniacha
Nakumbuka bado:-
"Habari yako mrembo
Nzuri kwa heshima ulijibu
Tukajuana
Uliniambia lako jina
Hawah Khadija, mwana wa mzee Suleiman
Bashasha nikajawa na furaha
Kwenu Arusha uliniarifu
Nako huku Dar kulikuwa yako mara ya mosi
Tena na kumbuka ulikuwa Juma mosi
Tukiwa tu twapozi
Salama kujuana
Kidogo twafaana
Moyo kauteka siwezi kana
Nitamani niwewako Sana
Ulivyo mzuri msichana
Moyo ukawa wakutojizuia
Nambari ya simu niliuliza
Lakini kumbe haukuwa na rununu
Ni zako picha
Picha zimebaki kumbukumbu
Yani na shangaa mbona...
Haukuwa nayo
Angalau nikuambie hallow
Baada ya kukupiga picha
Mie karibu naja huko Arusha
Kidogo nilienda biashara Moshi
Lakini akilini haitoki picha
Kukutafuta sitakoma
Pengine uhai kugoma
Mie kiberiti nawe mushuma
Mjini nasimama
Soko ni subiri
Wako urembo kunipofua jicho,
Mboni kuuona mwanga
Ama ulikuwa pepo
Binadamu malaika pengine
Silali naamsha popo
Kama jini nikatolewe mapepo
Natizama ramani ya Google
Ilenge kwa mzee Suleiman (wako mzazi)
Nikaribie angalau sauti...
Harufu yako kunivuta...
Nitimize ndoto(nikupate)
Wangu Bitoto(nikumbate)
Niwenawe zaidi ya picha(mie nawe mapacha)
Nipate tiba, timamu
Nisahau kicha
Nikutizame usiku mchana
Wimbo nikuimbie...zeze nikupige
Michoro nikuchore
Picha kamwe nikupige
Yaani umefanya Hadi:-
Ukutani picha
Chumbani...
Akilini...
Niyako picha.
Poem no.4
P.I.C.H.A
Series : pieces of love
By artyst msafih poetics
Msafih inks present ®
28th February2021
Typed on 31st March
STRIDA and poetic sol afrika
Msafih visual diaries Fliq
©2021
Author_ Analysis
It's all about a picture where by I met you in a town in Tanzania called Arusha but you had no phone. I only had to take photos of you, I still look for you but I can't find. I am still searching for you even on Google maps, lolwaiting to see you.
Post a Comment