Header Ads

ROMANTICISM: "NAOGOPA" BY MATYR

Niliambiwa ni kama nuru gizani,
Nasikia yanaleta furaha moyoni,
Mama alisema yanakuja na amani,
Sikatai mapenzi ni ya roho sabuni.

Sipingani, wewe ni chema chombo,
Kuanzia kwa miguu hata na umbo,
Ukweli, hakuna wa kukuzidi urembo,
Beautiful, hata nakusemea kimombo.

Unasema utanitunza kama yako mboni,
Eti utanionyesha mimi ni wa thamani,
Uhakika unamshinda Mildred mwandishi?
Mwenye kuvumilia kama shemeji Karushi.

Moyo unaogopa lakini mwili unataka,
Vipi kama Elinah kwa dharau ukanitoka?
Sagini si alinichezea kipanya kipaka,
Simsahau Ayieta, drama za anua anika.

Si kweli kuwa sipendi uhusiano na wewe,
Nasema, mimi sitaki kutembea na wewe,
Naogopa njiwa kuna siku utageuka mwewe,
Unipe mawazo kibao pombe ninywe nilewe.

MATYR✍️
(The Rich Pen)
@Art Place Kenya 🇰🇪

The bard appreciates the beauty of a woman who claims to love him, but tells her that he fears falling in love with her because of the past experiences he had with his ex-lovers.

No comments

Powered by Blogger.